Psalms 132:11-12


11 a Bwana alimwapia Daudi kiapo,
kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:
“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe
katika kiti chako cha enzi,

12 bkama wanao watashika Agano langu
na sheria ninazowafundisha,
ndipo wana wao watarithi
kiti chako cha enzi milele na milele.”

Copyright information for SwhKC